×
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii KAPs-Mafinga anayofuraha kuwatangazia kufunguliwa kwa dirisha la usajili kwa mwaka wa masomo 2024/2025. Kwa Level ya Astashahada (Certificate) na Stashahada (Diploma).
KATIKA FANI ZA
- Maendeleo Ya Jamii
- Ustawi wa Jamii
- Kilimo
SIFA ZA MUOMBAJI Kwa ngazi ya Cheti katika fani ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii awe amehitimu kidato cha Nne na Kupata ufaulu wa alama D nne isipokuwa masomo ya dini, na kwa fani ya Kilimo awe amepata ufaulu wa alama D nne lakini D mbili ziwe kutoka masomo ya sayansi (Physics, Biology, Chemistry, Geography, Mathematics, Nutrition, Agriculture)
Kwa ngazi ya Stashahada awe amehitimu Kidato cha Sita na kupata Principla Pass Moja (yaan D) na Subsidiary Moja (yaan S) au awe amehitimu na kupata Basic Technician Certificate kutoka katika chuo kinachotambulika na serikali.